Sunday, April 5, 2020

HOLY SPIRIT: By: Ev. Ladislaus Thadeus


ROHO MTAKATIFU  /  HOLY SPIRIT  By: Ev. Ladilaus Thadeus






Namshukuru MUNGU katika Utatu Mtakatifu aliyetuunganisha tena kwa njia hii (ya mtandao).

Naamini Roho wa MUNGU amekuwa kiongozi katika kundi hili tangu wazo la kuunda hii platform mpaka leo.



Kama tunavyojua si rahisi siku zote kumuelezea MUNGU kutokana na infinity yake yaani kutokuwa (kwake) na mwanzo wala mwisho kwa kutumia akili zetu ambazo ni absolutely limited, yaani zenye mipaka. Yale tunayojitahidi kuelekezana ni yale tu ambayo kwa huruma yake, yaani Divine Mercy, amependa kutufunulia; na kwa hakika tunayoyajua ni kidogo mno ukilinganisha na tusiyoyajua. Basi tumshukuru kwa hayo ambayo amependa kutufunulia na atakayoendelea kutufunulia.

Angalau kwa kifupi tukitaka kupata picha ya somo hili tuligawanye katika sehemu kadhaa :-



A : ROHO MTAKATIFU KABLA YA BIBLIA 

Ni wazi Biblia ni kitabu kichanga mno duniani. Maisha yalikuwepo na yaliendelea kuwepo kabla ya ufunuo huu. Biblia ni zawadi ya MUNGU kwetu na ni sanaa takatifu ya MUNGU kupitia wanadamu. Na hii ni kazi mojawapo kati ya nyingi za ROHO Mtakatifu. Kwa hiyo ROHO Mtakatifu alikuwepo akiwaongoza watu aliowachagua.

Kwa hiyo leo hii hata ukitunyang'anya Biblia bado huwezi kutunyang'anya ROHO Mtakatifu. Hivyo ni muhimu mno kujenga urafiki na ROHO Mtakatifu.



B : ROHO MTAKATIFU KATIKA AGANO LA KALE

Kitabu cha (Kutoka), yaani EXODUS kinaanza na stori ya mateso ya Waisrael kule Misri na kinahitimishwa na stori ya kuongozwa na ROHO Mtakatifu. Katika safari nzima ya kutoka Misri kwenda Kanaani ni habari ya kuongozwa na ROHO Mtakatifu kwa njia ya wingu wakati wa mchana na nguzo ya moto wakati wa usiku. Hii maana yake MUNGU analiongoza Taifa lake (Theocracy) kwa njia ya ROHO wake. Hapa unajengwa msingi imara kwa ajili ya INJILI yaani katika nyakati timilifu MUNGU hataliongoza Kanisa kwa ishara ya wingu au nguzo ya moto au TORATI, bali kwa njia ya ROHO Mtakatifu.
Atamuongoza kila mtu kwa sheria inayoandikwa katika vibao vya mioyo.



C : KATIKA AGANO JIPYA 

ROHO Mtakatifu anaendeleza kazi yake kwa Elizabeti, mama wa Yohana Mbatizaji na kwa Bikira Maria mama wa YESU KRISTO. Rejea Injili ya Luka sura ya 1 na ya 2. Pia katika Injili ndugu/pacha (SYNOPTIC GOSPEL), yaani Mathayo, Marko na Luka, katika sura ya 4 kuna ushahidi wa ROHO Mtakatifu katika kumuongoza Yesu kushinda vishawishi vya shetani katika kipindi ambacho Kristo alikuwa katika kilele cha kuumwa na njaa. Ni vizuri kujua wengi wetu huwa tunaongozwa na matakwa ya njaa na kupungukiwa kuliko kuongozwa na ROHO Mtakatifu. 

ROHO huyu mwema sana anajidhihirisha kwa Mitume na wafuasi wengine jumla yao 120 katika kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya 1 na katika huduma mbalimbali za Mitume katika kitabu kizima cha Matendo ya Mitume, na ndio maana kinaitwa kwa jina la Matendo ya Mitume. (ingawa historia inaonesha kulikuwa na mabishano kwa wanazuoni wa maandiko matakatifu kuwa kingeitwa matendo ya ROHO Mtakatifu.) Whatever the case, (Vyovyote vile iwavyo) muhimu ni kwamba ROHO wa MUNGU hutenda kazi kwa Kanisa lake na kwa yeyote apempendaye Yeye.



D : ROHO MTAKATIFU KATIKA MATENDO YA KILITRUJIA (CATHOLIC PERSPECTIVES)

He's really present and participating in the whole process to institute the Sacraments and Sacramental. Maana yake anawezesha mchakato mzima wa kuzifanya Sakramenti na Visakramenti viwepo.
Pia ROHO Mtakatifu huliongoza Kanisa katika nyanya zote.




E : ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA YA KILA SIKU.


Tapaswa kumruhusu Atuongoze, Atutawale, Atukemee, Atufariji, Atuonye, Atufundishe, Atuimarishe, Atujaze, Atubadilishe. Zaidi ya yote afanye atakavyo Yeye. Na hapa katika kufanya atakavyo Yeye ndio kuna muziki(kazi) mzito. Wengi wetu hapa ndio tunaanza kupoteana. Tunakwepa wajibu. Tunaruhusu uoga na standards za dunia zitutawale. Mungu atusaidie tushirikiane na huyu Rafiki Mwema ROHO Mtakatifu ayasimamie maisha yetu. Kazi yake kuu ni kudhihirisha Pendo la MUNGU Baba mioyoni mwetu kwa njia ya Kristo na hivyo tunapata utoshelevu wote na hivyo kuweza kumuita MUNGU wetu "ABA" yaani "BABA" (Rum 8:14-15)




                                

(Ufuatao ni ufupisho kutoka kwenye audio kuhusu Karama za ROHO Mtakatifu)


KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU
Kuna karama mbalimbali za Roho Mtakatifu kaa inavyoelezwa katika kitabu cha 1 Wakorintho 12:4-11. 



Makundi mbalimbali ya Karama

1. Karama za Utakaso (Sanctifying gifts)
Isaya 11:2  Vipaji 7 vya ROHO Mtakatifu
> Hekima
> Maarifa
> Shauri
> Uchaji wa MUNGU

> Nguvu
> Akili

> Ibada



2. Karama za Sala (Prayer Gifts)
> Kunena kwa Ndimi/Lugha
> Tafsiri ya Lugha
> Kutoa Unabii

Kitabu cha 1 Wakorintho sura ya 14 inaelezea kwa undani kuhusu namna gani ya matumizi ya karama ya kunena kwa lugha.

Matendo 2:4-8 



3. Karama za Neno
> Unabii
> Ushauri
> Neno la Maarifa
> Neno la Hekima

> Kufundisha
> Kuhubiri 
> Kutafsiri Lugha



4. Karama za Uponyaji
> Huruma (Compassionate)
> Kusikiliza (Listening)
> Mateso
> Kuponya 




5. Karama za Utawala
> Uongozi
> Utawala
> Masaidiano




6. Karama za Ubunifu
> Uchoraji
> Uchongaji
> Muziki

> Uchezaji > Mapambo
> Mapishi
> Ubunifu wa mitindo/majengo/michezo
> Uandishi




7. Karama za Nguvu
> Imani
> Uponyaji
> Kutenda Miujiza




8. Karama za Mafunuo
> Neno la Maarifa
> Neno la Hekima
> Kupambanua Roho




9. Karama Zilizo Zaidi ya Kawaida (Extra Ordinary)
> Kuonekana sehemu zaidi ya moja kwa wakati mmoja       (Bilocation) - Mt. Padre Pio
> Kuelea angani (Levitation) - Mt. Francisco

> Madonda ya YESU (Stigmata) Mt. Padre Pio





Hitimisho:
- Karama zote ni muhimu, na hakuna ambayo ni yenye ukubwa kwa mwenzake lakini karama iliyo kuu ni UPENDO.
- Mtu yeyote anaweza kupata karama

- Kiburi ni kikwazo kikuu katika kupokea karama.
- Njia rahisi kabisa ya kupokea karama kutoka kwa ROHO Mtakatifu, ni kuomba kwa imani.
- MUNGU anaweza kumpa yeyote karama kadiri anavyopenda.
- MUNGU huchunguza nia ya mtu kabla ya kumpa karama.






Digital Fellowship  -   April, 2020

1 comment:

Unknown said...

Atukuzwe Mungu Milele . Kazi nzuri mnaifanya ya kuujenga Ufalme wa Mungu kupitia hii blog .

COVID-19 Prayer Campaign

Catholic News Links

Catholic News Links
EWTN, Vatican News Swahili, CNA, CHARIS, Catholic Online, Church POP, Catholics Come Home